Jumatano 19 Novemba 2025 - 22:12
Waisraeli Wafanya Doria Kwenye Vijiji vya Syria: Mfumo Mpya wa Uvamizi wa Kimya Kimya

Hawza/ Ripoti zinaonesha ongezeko kubwa la shughuli za anga na ardhini zinazofanywa na jeshi la Israel kwenye maeneo kadhaa ya kusini mwa Syria.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ripoti zinaonyesha ongezeko kubwa la shughuli za anga na ardhini za jeshi la Israel katika maeneo kadhaa ya kusini mwa Syria, ambapo tukio la hivi karibuni ni uvamizi wa doria ya kijeshi katika kijiji cha “Sayda al-Jawlaan” katika vitongoji vya kusini vya Quneitra.

Katika utulivu ambao unaonekana kana kwamba ni utulivu kabla ya tufani, magari matano ya kijeshi ya Israel yaliingia katika kijiji cha Sayda al-Jawlaan kwenye eneo la mbali zaidi kusini mwa Quneitra huko Syria; kana kwamba walikuwa wakitembea katika ardhi isiyo na wenyewe. Vikosi hivyo vilisimama katika barabara ya vumbi na kuweka kituo cha ukaguzi cha muda katika mlango wa kuingia kijijini.

Walianza kukagua watu wanaopita na kuangalia vitambulisho vyao; tukio linaloonesha si tu kupuuzwa kwa mipaka, bali pia kutokuwepo kabisa kwa nguvu yoyote inayoweza kuzuia uvamizi huu wa mara kwa mara.

Masaa machache tu kabla ya hili, magari mawili ya kivita yalielekea katika vitongoji vya mji wa “Koya” katika bonde la Yarmouk na yakaanza kufyatua risasi ovyo, kisha yakapita kuelekea kambi ya “al-Jazira” ambayo kwa sasa imegeuka kuwa kituo cha kudumu cha majeshi ya Israel.

Mabadiliko ya kimkakati: Kudhibiti uvamizi wa kimya kimya

Kinachoendelea kusini mwa Syria si jambo la kupita, wala hakipaswi kufasiriwa tu kama harakati rahisi za kijeshi za kimbinu; tukio hili lina maana pana kuliko linavyoonekana. Kiwango cha hatua hizi hakipimwi kwa vipimo vya kukiukwa mipaka ya jadi, bali ni kuongezeka kwa mfumo mpya wa mkusanyiko wa kijeshi unaoonesha kuwa utawala huu uko mbioni kuweka msingi wa uvamizi wa kimya kimya na usiotangazwa.

Zana laini: Ukusanyaji wa taarifa za kijamii

Mabadiliko haya ya kimkakati yanaambatana na nguvu laini ambayo sasa imekuwa imara kama tu nguvu yao ya kijeshi. Wakati mizinga na wanajeshi wanatembea katika vijiji vilivyo vya majirani, wanatumia pia zana zao laini kupitia dodoso zinazogawiwa kwa wakazi. Wanajeshi wavamizi huwauliza wenyeji kuhusu idadi ya wanakaya, kazi zao, hali ya afya, kipato, vyeti vya elimu na hata mahitaji yao ya chakula, na wanauliza pia mtazamo wao kuhusu “mamlaka mpya”.

Hatua hii ina maana ya kukusanya data kamili za kijamii katika maeneo ambayo kwa hakika yako chini ya ushawishi wa wavamizi; katika vijiji kama vile al-Hameediyya, al-Qahtaniyya, Rasm al-Rawazi, Rasm al-Bayda, Rasm Abu Shabta na vijiji vingine ambavyo vimekuwa eneo wazi kwa doria za kijeshi.

Kwa njia hii, taratibu kusini mwa Syria, ramani mpya zinachorwa; ramani ambazo hazitangazwi kwenye makongamano, bali zinachukuliwa kupelekwa ardhi nyengine; mahali ambapo wavamizi wanaunda mfumk mpya ambao haupeperushi bendera, bali kwa ukimya, unabadilisha ardhi na kubadilisha utambulisho wa wakazi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha